Wewe na Pesa, Je Pesa na Wewe?
Wewe na Pesa, Je Pesa na Wewe?
Couldn't load pickup availability
“Wewe na Pesa, Je Pesa na Wewe?” ni kitabu cha kipekee kinachowapa wasomaji maarifa ya kina kuhusu mbinu za kuunda mfumo wa kuwa na kipato endelevu—hata ukiwa katika mazingira magumu ya kiafya au kiuchumi. Kitabu hiki kinaeleza kwa kina tabia za pesa na kwa undani jinsi mtu anaweza kujenga mfumo wa kutengeneza pesa endelevu. Ni maarifa au elimu mpya ambayo haifundishwi mashuleni au vyuoni , hivyo kinahitajika kwa kila mtu yeyote anayehitaji kuwa na miundombinu ya kuwa na pesa endelevu.
Kupitia maarifa ya kiutendaji, mifano halisi, na mbinu bunifu, msomaji ataweza:
- Kutambua tabia za pesa unazopaswa kujua kwa ustawi wa kipato
- Kujenga mfumo wa kifedha unaojitegemea na kuhimili changamoto za maisha.
- Kuelewa uhusiano wa kihisia na pesa, na jinsi ya kuubadilisha kuwa chanya.
- Kupanga mikakati ya kifedha inayozingatia afya bora, kufurahia maisha, na uendelevu wa kipatao
Kitabu hiki ni hazina kwa vijana, wajasiriamali, wazazi, na yeyote anayetamani kujenga mfumo wa PESA NA WEWE na sio wewe na pesa: Je, pesa inakufuata kama unavyoifuata wewe?
